Mfalme Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kuliko wote ulimwenguni. Anatushauri, Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu (Mithali 25:21-22). Yesu anasema jambo fulani linalofanana sana na hilo katika mafundisho Yake yaliyofuata (Mathayo 5:44-45). Kitendo cha kutukanwa, kupigwa, kushtakiwa au kulazimishwa kubeba mzigo mzito usio wa kwako kinaweza kusababisha mafutu mabaya kabisa katika asili ya binadamu. Yaani, chuki, hasira, ukatili na hata vurugu. Lakini pale wale waliobarikiwa kuwa na hekima wanapojikuta katika majaribu makubwa kama hayo tabia yao haitakiwi kuwa ya shari, inda au ya kulipiza kisasi. Bali inatakiwa kuwa ya kusaidia, kuwa na ridhaa ya kutenda mambo mema, na kuwa mwema kwa wengine siku zote.
adui
adversity
anger
bitterness
blessings
bwana
chakula
chaos
chuki
cruelty
doctrine
embers
enemy
food
fussiness
good
hasira
hatred
heavy-load
hekima
hunger
inda
jesus
king-solomon
kisasi
kiu
lord
mafundisho
mafutu
majaribu
maji
makaa-ya-moto
mathayo-5-44-45
matthew-5-44-45
mema
mfalme-sulemani
mithali-25-21-22
mzigo-mzito
njaa
proverbs-25-21-22
revenge
shari
teachings
thawabu
thirsty
trials
ukatili
vurugu
water
wisdom
yesu
About This Quote
About Enock Maregesi
Enock Maregesi.